Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

TASAC yaendelea kunoa Mabaharia kupitia Mtihani wa Mahojiano.

Imewekwa: 11 June, 2024
TASAC yaendelea kunoa Mabaharia kupitia Mtihani wa  Mahojiano.

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kupitia Kurugenzi ya Usalama, Ulinzi na Utunzaji wa Mazingira (DMSE) leo tarehe 10 Juni, 2024 katika jengo la PSSSF Tower jijini Dar es Salaam limefanya ufunguzi wa Mitihani ya Mahojiano kwa ajili ya maafisa wa Meli “Oral examinations” ufunguzi huo umehusisha wajumbe wa  Bodi ya Watahini (Board of Examiners), wawakilishi wa watahiniwa (Engine and Deck Officers) na waangalizi (Observers). 

Aidha, Mkurugenzi wa Usalama, Ulinzi na Utunzaji wa Mazingira (DMSE), Bi. Leticia Mutaki aliwashukuru wadau wote waliohudhuria na kwa kipekee kabisa amewapongeza Bodi ya Watahini kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kushirikiana na TASAC katika usahili wa mahojiano wa maafisa. 

"TASAC inatambua na kuthamini mchango wenu katika sekta hii ya usafiri na usafirishaji kwa njia ya maji, mmekuwa nguzo imara katika kuhakikisha zao linalotokana na watahiniwa hawa linakuwa lenye viwango vya juu kabisa vya kimataifa." Ameongeza Bi. Leticia.

Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu Bw. Nahson Sigala ambaye ni Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi (TASAC) amefungua kikao hicho kwa kuwashukuru na kuwapongeza watahiniwa  kwa kukidhi vigezo vya kufanya mitihani hiyo ambayo hufanyika mara nne (4) kila mwaka. Watahiniwa mbalimbali katika sekta ya ubaharia hufanyiwa usahili wa mahojiano kwa lengo la kupata maafisa waongoza Meli na wahandisi wa Meli wenye vigezo na viwango vya Kimataifa katika uongozaji wa Meli kwa mujibu wa Mkataba wa Kimataifa wa Mafunzo,utoaji vyeti na ufanyaji kazi kwa Mabaharia (STCW) 1978 .

Mrejesho, Malalamiko au Wazo