Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

BOTI YA KISASA KURAHISISHA UOKOZI NA MATIBABU UKANDA WA ZIWA - RC MTANDA

Imewekwa: 21 July, 2025
BOTI YA KISASA KURAHISISHA UOKOZI NA MATIBABU UKANDA WA ZIWA - RC MTANDA

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda leo julai 07, 2025 amekagua Meli ya Kisasa ya Uokozi na Matibabu iliyojengwa chini ya mradi wa Kikanda wa Usafiri na Mawasiliano Ziwa Victoria unaojumuisha nchi ya Tanzania na Uganda.

Akizungumza wakati wa ziara yake hiyo kutoka bandari ya Kaskazini na kurudi Mhe. Mtanda ameishukuru Serikali ya Awamu wa Sita chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuona umuhimu wa kuwekeza kwenye eneo la Ziwa Victoria ili kuhakikisha wananchi wake wanakua salama wanaposafiri na kufanya shughuli za kiuchumi ikiwemo uvuvi.

"Tunashukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa utekelezaji wa mradi huu ambao unakaribia kukamilika na moja ya mambo yaliyo chini ya mradi huu ni pamoja na kuweka mawasiliano na kujenga kituo cha Kikanda cha kuratibu shughuli za utafutaji na uokoaji kilichopo Ilemela na ununuzi wa boti hii pamoja na boti mbili ndogo za utafutaji na uokoaji,” amesema Mhe. Mtanda.

Aidha, amesema boti hiyo ya kisasa italeta fursa kwa wagonjwa watakaopata dharura zozote majini itawafikia kwa haraka na kutoa matibabu ya dharura kabla ya nchi kavu kwa ajili ya kupelekwa hospitali ya rufaa katika eneo husika.

Nahodha wa Boti hiyo Naho. Grayson Mwarwa amesema boti hiyo ina uwezo wa kulaza wagonjwa wanne kwa mara moja pamoja na wengine 12 wakihudumiwa kwa wakati huo huo na kwamba ina huduma ya kuongeza hewa ya Oksijeni kwa wagonjwa.

Kwa upande wake Afisa Mfawidhi wa Mkoa wa TASAC Mwanza Bw. Joseph Mkumbo amesema boti hiyo ya kisasa ina uwezo wa kutembea maili 18 kwa saa.

Aidha, ameongeza kuwa TASAC tayari wameifanyia majaribio na kuonesha mafanikio makubwa sana kwa kwenda na kurudi Ukerewe kwa kasi kubwa.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo