TASAC WAPIGWA MSASA MFUMO WA PEPMIS

Menejimenti na Watumishi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) wamepatiwa mafunzo ya Mfumo wa Utendaji kazi wa Watumishi (PEPMIS - Public Employee Performance Management Information System), leo tarehe 14 Februari 2025 ikiwa ni muendelezo wa mafunzo ya namna ya kutumia mfumo huo kwa watumishi wa umma hapa nchini.
Akiwakaribisha wawezeshaji kutoka Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Huduma za Shirika, Bw. Hamid Mbegu amewaasa watumishi kutumia mafunzo hayo kwa ajili ya kuboresha ujazaji wa taarifa katika mfumo wa PEPMIS.
Kwa upande wake, Meneja wa Rasilimali Watu, Bi. Pili Mazowea amesema kuwa mafunzo hayo ni endelevu kwa watumishi ili kujikumbusha na kutatua changamoto zinazowakabili wakati wa kujaza utendaji kazi katika mfumo huo.
TASAC imekuwa ikitoa mafunzo kwa watumishi kuhusu namna ya kujaza utendaji kazi katika mfumo huu ambao umeanzishwa ili kuongeza ufanisi na uwajibikaji kwa watumishi wa Umma.