TASAC KUSHIRIKI MAONESHO YA SABASABA
TASAC KUSHIRIKI MAONESHO YA SABASABA
Imewekwa: 14 July, 2023

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania, TASAC linashiriki katika maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa.
Maonesho hayo yenye Kauli Mbiu:- “Tanzania: Mahali Sahihi Pa Biashara na Uwekezaji”, yameanza tarehe 28 Juni, katika viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam na yatahitimishwa tarehe 13 Julai 2023.
Lengo la kushiriki maonesho hayo ni kujenga uelewa na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kazi na majukumu yanaotekelezwa na TASAC kwa mujibu wa Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania, Sura 415 na mabadiliko yake.
TASAC inawaalika wananchi wote kutembelea maonesho haya na kufika katika banda la TASAC lililopo katika ukumbi wa Karume banda namba 22 na 23.
12 September, 2023
TASAC yafanya semina ya kutoa elimu kwa kamati ya kudumu ya sheria ndogo ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzani
16 August, 2023
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TASAC Nahodha. Mussa H. Mandia atakuwepo kwenye Kikao Kazi cha Msajili wa Hazina na Wenyeviti na Watendaji Wakuu wa Taasis za Umma