Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

TASAC na Wizara ya Uchukuzi kushiriki kikao kifupi cha Kamati ya maandalizi ya Semina ya Kanda ya Afrika ya Usalama wa Vyombo vya Usafiri kwa Njia ya Maji (AAMA))

Imewekwa: 23 April, 2024
TASAC na Wizara ya Uchukuzi kushiriki kikao kifupi cha Kamati ya maandalizi ya Semina ya Kanda ya Afrika ya Usalama wa Vyombo vya Usafiri kwa Njia ya Maji (AAMA))

Bi.Stella Katondo Mkurugenzi wa Usalama na Mazingira Wizara ya Uchukuzi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati akiwa katika kikao kifupi cha Kamati ya maandalizi ya Semina ya Kanda ya Afrika ya Usalama wa Vyombo vya Usafiri kwa Njia ya Maji  kilichofanyika leo tarehe 15 Aprili, 2024 kwa kushirikiana na wawakilishi kutoka Shirika la Bahari Duniani (IMO), Mkurugenzi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC) Bw. Salum Mohamed na Menejimenti ya TASAC katika kikao cha mwisho cha Maandalizi ya Semina hiyo inayotarajiwa kufanyika tarehe 16 - 17 Aprili, 2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa JNICC, Dar es Salaam. 

Nchi mbalimbali kutoka Afrika zinazojishughulisha na Usafiri kwa njia ya Maji zinatarajiwa kushiriki katika Semina hiyo ikiwemo Afrika Kusini, Nigeria, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kenya, Uganda, Ghana na Gabon.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo