Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

TASAC kueendesha kikao cha 7 cha Nchi za Afrika Mashariki zinazojihusisha na Usimamizi wa shughuli za Bahari (AAMA)

Imewekwa: 23 April, 2024
TASAC kueendesha kikao cha 7 cha Nchi za Afrika Mashariki zinazojihusisha na Usimamizi wa shughuli za Bahari  (AAMA)

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limeendesha kikao cha 7 cha Nchi za Afrika Mashariki zinazojihusisha na Usimamizi wa shughuli za Bahari (Association of Maritime Administrations) kilichofanyika kwa njia ya mtandao siku yua Jumanne tarehe 26 Machi, 2024 katika Ukumbi wa kimataifa wa Mikutano wa Mwl. Julius Nyerere (JNICC) na kuongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Bw. Mohamed Salum.

Kikao hicho ambacho hufanyika kila mwaka na kuruhusu wanachama kujadili masuala mbalimbali ya usimamizi wa bahari, kinalenga pia maandalizi ya mkutano wa nchi hizo utakaofanyika mwezi Oktoba, 2024 ambapo Tanzania kupitia TASAC itakuwa Mwenyekiti wa mkutano huo.

AAMA ina wanachama sitini ambazo ni nchi za Afrika ikiwemo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo