Habari

Imewekwa: 09/04/2020

TASAC YAJIPONGEZA KWA KUHAKIKI MELI ZA MIZIGO 100

TASAC YAJIPONGEZA KWA KUHAKIKI MELI ZA MIZIGO 100

TASAC imeanza kufanya shughuli ya kuhakiki mizigo mnamo tarehe 17 Februari 2020 katika Bandari ya Dar es Salaam, kazi hii inahusisha uhakiki wa mizigo inavyopakuliwa na kupakiwa melini. Kimsingi TASAC imefanikiwa kufanya shughuli hii kwa masaa 24 pamoja na uchache wa wafanyakazi waliopo.

Mpaka kufikia tarehe 5 April 2020 TASAC imefanikiwa kuhakiki mizigo kwa Meli 100 kama ifuatavyo;

*Meli za shehena mchanganyiko (General Cargo) na kuhudumia meli 13 ambazo zilishusha mzigo wenye tani za ujazo 95,740.72.

*Meli za Kichele (Dry Bulk Cargo) na kuhudumia meli 15 ambazo zilishusha mzigo wenye tani za ujazo 365,709.80.

* Meli za Makasha (Container) kwa kuhudumia Meli 52 zenye makasha yaliyoingia nchini 37,755 na yaliyotoka 33,264.

*Meli za magari zimehakikiwa katika Meli 22 zenye tani za ujazo 22,002.

Aidha, TASAC imefanikiwa pia kuhakiki mizigo kwenye Bandari kavu moja ambayo ni KICD.