KATIBU TAWALA MKOA WA GEITA AIPONGEZA TASAC 
                        
                    
                
            
                    Katibu Tawala mkoa wa Geita Mohamed Gombati amepongeza Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kwa utoaji huduma bora ya udhibiti wa vyombo vya usafiri majini na uvuvi mkoani humo.
Ameyasema hayo tarehe 26 Septemba, 2025 wakati alipotembelea banda la TASAC katika maonyesho ya 8 ya teknolojia ya madini yaliyoanza tarehe 18 na kilele chake ni tarehe 28 Septemba, 2025 hapa Geita.
"Hongereni TASAC kwa kazi mnayofanya ya ukaguzi na udhibiti katika usafiri majini. Nashukuru  sana jinsi mlivyoshughuli changamoto za kisiwa cha Izmacheli maeneo ya  Nkome. Ushirikiano ni mzuri na unawafanya wananchi  wawe na imani na  ninyi". Amesema Gombati
 
Pia, Gombati ameahidi Serikali ya mkoa itaendelea kutoa ushirikiano na msaada wa karibu utakaohitajika kwa ajili ya kutatua changamoto ya matumizi ya vifaa okozi na kuhakikisha usafiri majini unaendelea kuwa salama ili kuwawezesha wananchi katika shuguli zao za kujipatia maendeleo.