Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

Taasisi za Umma zanolewa kujua uhitaji wa wataalamu wanaotakiwa katika taasisi zao.

Imewekwa: 18 January, 2024
Taasisi za Umma zanolewa kujua uhitaji wa wataalamu wanaotakiwa katika taasisi zao.

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limeshiriki kikao kazi cha kujengewa  uwezo na mbinu za kujua uhitaji wa wataalam katika taaasisi za Umma kwa kutumia Mfumo wa Tathmini ya Mahitaji ya Rasimali Watu Serikalini (Human Resources Assessment) yanayotolewa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni, mkoani Dar es Salaam.Mafunzo hayo yanatolewa kuanzia tarehe 14 hadi 16 Disemba, 2023.

Lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha menejimenti za taasisi kufanya uchambuzi wa watumishi wanaowahitaji kwa kila kada kulingana na majukumu na uzito wake kwa kila kitengo katika taasisi za Umma. Hayo yalizungumza na Bw. Mamboleo Mpugusi ambaye alikuwa ni mwezeshaji kutoka ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala bora. 

Bw. Mamboleo alisema "Mfumo huu utasaidia kuchambua mahitaji ya wataalam, kutambua mahali penye upungufu wa wataalam na kujua ziada ya wataalam waliopo na kada zao.

“Kila mwaka tunapokea maombi ya vibali vya kuajiri watumishi.Tumefahamu kuwa taasisi zinazojiweza kimapato watumishi wengi wanapenda kwenda huko". Aliongeza Bw. Mamboleo.

Taasisi zinazoshiriki mafunzo hayo ni pamoja na TASAC, Chuo cha Kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere (MNMA) na Tume ya Taifa ya (UNESCO) ambapo walengwa wa mafunzo ni Wakurugenzi, Mameneja na Wakuu wa Vitengo.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo