Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limeshiriki katika maonesho ya 6 ya Teknolojia ya Madini 2023.

Imewekwa: 07 October, 2023
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limeshiriki katika maonesho ya 6 ya Teknolojia ya Madini 2023.

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limeshiriki katika maonesho ya 6 ya Teknolojia ya Madini 2023.

Maonesho hayo yenye Kauli Mbiu: ”Matumizi ya Teknolojia Sahihi Katika Kuinua Wachimbaji Wadogo Kiuchumi na Kuhifadhi Mazingira”, yamefunguliwa na Naibu Waziri Mkuu Mhe. Dotto Biteko tarehe 20 Septemba,2023 katika viwanja vya Bombambili Mkoani Geita na  yatahitimishwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania tarehe 30 Septemba, 2023.

Lengo la kushiriki maonesho hayo ni kujenga uelewa na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kazi  na majukumu yanaotekelezwa na TASAC kwa mujibu wa Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania, Sura 415 na mabadiliko yake.

TASAC inawaalika wananchi wote kutembelea maonesho haya na kufika katika banda la TASAC ili kupata elimu zaidi kuhusu usafiri kwa njia ya maji.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo