Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limeshiriki katika maonesho ya 01 ya Huduma za BRELA na Wadau wake 2023.

Imewekwa: 30 October, 2023
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limeshiriki katika maonesho ya 01 ya Huduma za BRELA na Wadau wake 2023.

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limeshiriki katika maonesho ya 01 ya Huduma za BRELA na Wadau wake 2023.

Maonesho hayo yenye Kauli Mbiu: ” Urasimishaji wa biashara katika Mapinduzi ya Nne ya Viwanda”, yamefunguliwa rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Hashim Abdallah Komba Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila tarehe 24 Oktoba, 2023 katika viwanja vya Mlimani City jijini Dar es Salaam na  yatahitimishwa tarehe 27 Oktoba, 2023.

Lengo la TASAC kushiriki maonesho hayo ni kujenga uelewa na kutoa elimu kwa wadau kuhusu kazi  na majukumu yanaotekelezwa na Shirika hili kwa mujibu wa Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania, Sura 415 na mabadiliko yake.

TASAC inawaalika wananchi wote kutembelea maonesho haya na kufika katika banda la TASAC ili kupata elimu zaidi kuhusu usafiri kwa njia ya maji.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo