Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) likishirikiana na Shirika la Bahari Duniani (IMO) limetoa mafunzo ya uratibu wa utafutaji na uokoaji eneo la ajali majini.

Imewekwa: 28 April, 2023
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) likishirikiana na Shirika la Bahari Duniani (IMO) limetoa mafunzo ya uratibu wa utafutaji na uokoaji eneo la ajali majini.

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) likishirikiana na Shirika la Bahari Duniani (IMO) limetoa mafunzo ya uratibu wa utafutaji na uokoaji eneo la ajali majini tarehe 24 Aprili, 2023 Dar es salaam.

Akifungua mafunzo hayo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya ujenzi na uchukuzi Dkt. Ally Possi amesema wataalamu wa sekta ya Bahari wanahitajika kueleza changamoto zinazoikumba sekta hiyo hasa katika swala la uokoaji pale majanga yanapotokea.

Dkt. Possi ameongeza kuwa Taifa litapunguza kuaminiwa pamoja na kuhatarisha sekta nyingine ikiwemo sekta ya utalii endapo hatua stahiki za uokoaji zisipochukuliwa.

"Ni muhimu kutambua changamoto zinazokabili Taifa letu kwahiyo wadau mtumie mafunzo haya kuleta mapendekezo ya changamoto hizo kwa serikali na sisi tutazichukua na kuzifanyia kazi." Amesema Possi.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo