Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limeingia makubaliano ya mashirikiano ya usimamizi wa meli za uvuvi na Mamlaka ya Usimamizi wa Uvuvi wa Bahari Kuu(DSFA).

Imewekwa: 28 April, 2023
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limeingia makubaliano ya mashirikiano ya usimamizi wa meli za uvuvi na Mamlaka ya Usimamizi wa Uvuvi wa Bahari Kuu(DSFA).

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limeingia makubaliano ya mashirikiano ya usimamizi wa meli za uvuvi na Mamlaka ya Usimamizi wa Uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA) tarehe 05 Aprili, visiwani Zanzibar.

Katika makubaliano hayo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania Bw. Kaimu Abdi Mkeyenge amesema ni jambo jema taasisi kuwa na makubaliano haya ya kushirikiana katika Nyanja mbalimbali ikiwemo kubadilishana taarifa kuhusu meli husika na kufanya maamuzi shirikishi kuhusu usajili wa meli yoyote ya uvuvi katika eneo tengefu la uchumi nchini.

Aidha, Mkurugenzi Mkuu Mkeyenge ameongeza kuwa kupitia ushirikiano huo kutasaidia kushirikiana kwa kuiwezesha DSFA kuhakikisha inadhibiti uvuvi haramu, ambao haujaruhusiwa na usioratibiwa.

Mgeni rasmi katika makubaliano hayo alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Bi. Khadija Khamis Rajab.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo