Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

RC MBEYA AIPONGEZA TASAC

Imewekwa: 22 September, 2025
RC MBEYA AIPONGEZA TASAC

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe.  Beno Malisa mnamo tarehe 14 Septemba, 2025 alilipongeza Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kwa ufanisi wake katika kutoa elimu ya usalama majini na kusimamia sheria na kanuni.

Akizungumza wakati alipotembelea banda la TASAC katika ufunguzi wa Maonesho ya Biashara ya Nyanda za Juu Kusini (Kusini International Trade Fair).

Mhe. Malisa ameitaka TASAC kuongeza juhudi katika kutoa elimu kwa wananchi hususan wakazi wa maeneo ya Matema, Kyela na maeneo mwambao wa Ziwa Nyasa.

“Nawapongeza TASAC kwa kushiriki maonesho haya kwa kuzingatia ukanda huu ni mwambao wa Ziwa Nyasa wenye shughuli nyingi za uvuvi na usafirishaji kwa njia ya maji, endeleeni kusimamia kanuni na sheria ili kuhakikisha wananchi wanapata uelewa wa kutosha na wanakua salama,” alisema Mhe. Malisa.

Maonesho hayo yenye kaulimbiu “Amani Kwanza, Maendeleo Daima, Chagua Kiongozi Bora, Jenga Uwekezaji Imara Tanzania” yalianza rasmi tarehe 12 Septemba 2025 yanatarajiwa kufikia tamati tarehe 21 Septemba 2025.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo