Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

Naibu waziri Uchukuzi aitaka TASAC kuhakikisha boti yenye vifaa muhimu vya matibabu unakamilika kwa wakati na viwango.

Imewekwa: 18 January, 2024
Naibu waziri Uchukuzi aitaka TASAC kuhakikisha boti yenye vifaa muhimu vya matibabu unakamilika kwa wakati na viwango.

Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi David Kihenzile amelitaka Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kuhakikisha mradi wa ujenzi wa boti yenye vifaa vya matibabu (Ambulance Boat) unakamilika kwa wakati na viwango ili kuwawezesha wakazi wa Ziwa Viktoria na visiwa vyake kuanza kutumia huduma hizo.
 
Akizungumza wakati wa utiaji saini mkataba huo baina ya TASAC na Kampuni ya LOCA Muhendislik Gemi Mak. PLas Ve Gd. San Tic ltd Sti ya nchini Uturuki Naibu Waziri Kihenzile amesema kukamilika kwa mradi huo utakuwa kichochea kikubwa kwa wakazi hao kupata huduma za afya na hivyo kuongeza usalama.
 
 
“Mradi huu ni wa muhimu sana na umekuja wakati muafaka wakati Serikali ikiendelea kuwekeza katika ujenzi wa miundombinu hivyo hakikisheni mradi huu unakamilika kwa wakati ili wananchi wananchi hawa waendelee kupata huduma kupitia boti hii”
 
Naibu Waziri Kihenzile ameongeza kuwa Serikali iko katika hatua mbalimbali za utekelezaji wa mradi wa ya kujenga kituo cha Utafutaji na Ukoaji ambacho kitafanya kazi kwa ushirikiano na kituo cha Dar es Salaam ili kuimarisha usalama katika usafiri majini.
 
Naye Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Bi. Amina Makilagi ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuimarisha usafiri huo kwa kuwekeza katika ujenzi wa meli na maboresho ya miundombinu lengo likiwa kuchagiza uchukuzi.
 
Mkuu wa Wilaya Makilagi ameongeza kuwa mradi huu umekuja wakati muafaka kwani kukamilika kwake kutachangia kuokoa maisha ya wananchi kwani watapata huduma hiyo kwa wakati.
 
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya TASAC Nahodha Musa Mandia amemuhakikishia Naibu Waziri Kihenzile kuwa Bodi na Menejimneti zimejipanga kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati na viwango.
 
Mradi wa Ujenzi wa boti ya yenye vifaa vya matibabu unaotekelezwa na kampuni ya Kampuni ya LOCA Muhendislik Gemi Mak. PLas Ve Gd. San Tic ltd Sti ya unatarajiwa kugharimu takribani shilingi bilioni nne na unatawajiwa kukamilika ndani ya kumi na nne(14).

Mrejesho, Malalamiko au Wazo