Naibu Katibu Mkuu (Uchukuzi) afanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Uchukuzi Mhe. Dkt. Ally Possi ameongozana na watendaji wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) leo tarehe 3 Juni, 2024 katika ziara iliyofanyika Bandari ya Dar es Salaam.
Lengo la ziara hiyo ni kuona namna shughuli za bandari zinavyoendelea kwa kuzingatia kanuni, taratibu na sheria ikiwa ni pamoja na kuangalia utekelezaji wa maelekezo yanayotolewa na Serikali kupitia TASAC ambayo ni taasisi ya udhibiti wa huduma za bandari.
Dkt. Possi amesema kuwa Serikali imewekeza katika miundombinu ya bandari hivyo ni jukumu la Wizara kufuatilia utekelezaji wa shughuli mbalimbali bandarini hapo.
"Serikali imewekeza katika miundombinu ya bandari ili kuongeza pato la taifa, hivyo sisi kama Wizara tumeona tutembelee Bandari na kujionea namna shughuli zinavyoendelea,amesema Dkt.Possi.
Aidha, ameongeza kuwa kupitia ziara hii wamepata fursa ya kuona namna ambavyo Mamlaka ya Bandari (TPA) kukabidhi shughuli za kibandari kwa wabia ambao ni DP World Dar es Salaam.
Bandari ya Dar es salaam ni lango la biashara kwa Tanzania pamoja na nchi jirani kama Rwanda,Burundi, DRC Congo,Zambia na Malawi