Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TASAC afanya ziara Meli ya MV Mwanza ''HAPA KAZI TU''.

Imewekwa: 18 January, 2024
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TASAC afanya ziara Meli ya MV Mwanza  ''HAPA KAZI TU''.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Nahodha. Mussa Mandia pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Wakili Mohamed Salum wamefanya ziara ya kutembelea Meli ya Mv Mwanza 'Hapa Kazi Tu' inayotarajiwa kufanyiwa majaribio majini Machi, 2024.

Ziara hiyo ilikuwa na lengo la kukagua mradi huo ambao unatarajiwa kukamilika hivi karibuni.

" Kwa niaba ya Bodi na Menejimenti ya TASAC kwa ujumla tumefarijika kwa nafasi, tumeweza kujionea kilichofanyika na kwa maelezo niliyoyapata ni asilimia 92 ya ujenzi umekamilika." Amesema Nah. Mandia.

Aidha, Nah. Mandia amewapongeza Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) kwa kazi kubwa ya usimamizi wa ujenzi wa Meli hiyo.

" Nitumie fursa hii kuwapongeza kwa kazi kubwa mliyofanya, endeleeni kufanya hivyo kwa nia ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma iliyokusudiwa kutokana na uwekezaji uliofanya na serikali. " Amesema Nah. Mandia.

Kwa upande wa Meneja Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) Bw. Anselm Namala amesema kuwa amefarijika kupokea ugeni huo na kuahidi kufikia mwezi Machi na Aprili yatafanyika majaribio ya Meli hiyo kwenye maji.

"Nimefarijika kupokea ugeni wa Bodi ya TASAC ambao wamekuja kutembelea mradi huu na kuona maendeleo yaliyopo katika ujenzi, Meli yetu iko Asilimia 92 ya ujenzi, kati ya mwezi Machi na Aprili, 2024 tutafanya majaribio ya kwenye maji (Sea Trial) na kati ya mwezi Mei, 2024 tutakabidhiwa Meli na Mkandarasi." Amesema Bw. Namala.

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bi. Rukia Shamte pamoja na Menejimenti ya TASAC pia wameshiriki  ziara hiyo ya kutembelea mradi wa Meli ya Mv Mwanza "Hapa Kazi Tu" ambayo imefanyika tarehe 22 Desemba, 2023 jijini Mwanza.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo