Wajumbe wa Menejimenti ya TASAC washiriki mafunzo ya usimamizi wa viashiria hatarishi katika Shirika
Wajumbe wa Menejimenti ya TASAC washiriki mafunzo ya usimamizi wa viashiria hatarishi katika Shirika
Imewekwa: 24 May, 2024
Wajumbe wa Menejimenti ya Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania - TASAC wakiwa katika mafunzo kuhusu masuala mbalimbali ya usimamizi wa viashiria hatarishi katika Shirika. Mafunzo hayo ya siku tatu yanajikita katika kutambua vihatarishi vilivyopo, namna ya kudhibiti pamoja na namna ya kukabiliana navyo pale vinapotokea bila kuathiri utendaji kazi wa kila siku.
Mafunzo haya yanayofanyika Shule ya Uongozi Mwalimu Nyerere, Kibaha yameanza leo tarehe 23 Mei hadi 25 Mei, 2024.