Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

Mkurugenzi Mkuu wa TASAC ashiriki Kongamano la Tatu la Uchumi wa Buluu, jijini Dar es Salaam

Imewekwa: 04 July, 2024
Mkurugenzi Mkuu wa TASAC ashiriki Kongamano la Tatu la Uchumi wa Buluu, jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania  (TASAC ) Bw. Mohammed Salum ameshiriki katika Kongamano la Tatu la Uchumi wa Buluu ambalo limefanyika leo tarehe 4 katika Kituo cha  Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam. 

Kongamano hilo limejumuisha wadau mbalimbali wa Sekta ya Usafiri Majini ikiwemo Umoja wa wanawake walio katika sekta ya Usafiri Majini katika Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika (WOMESA), Azam Marine, Zan Fast Ferries na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA).

Kongamano hilo la Siku mbili lenye Kauli Mbiu ya "Kuunganisha Usalama Baharini, Utunzaji wa Mazingira na Maendeleo ya Teknolojia kwa ajili ya Ukuzaji wa Uchumi wa Buluu, linatarajia kuhitimishwa kesho tarehe 05 Julai, 2024.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo