Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

Mkurugenzi Mkuu wa TASAC aendesha kikao cha wadau wa usafiri  majini jijini Mwanza

Imewekwa: 29 May, 2024
Mkurugenzi Mkuu wa TASAC aendesha kikao cha wadau wa usafiri  majini jijini Mwanza

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC)  Bwn. Mohamed Malick Salum  ameendesha kikao cha watoa huduma, waendeshaji na wadau wa usafiri  majini, kilichofanyika leo tarehe 28 Mei, 2024 katika Ukumbi wa Mamlaka ya USimamizi wa Bandari jijini Mwanza.

Katika kikao hicho,  Bwn. Mohamed amewapongeza wadau hao kwa juhudi wanazoonyesha katika kukidhi matakwa ya leseni ya kazi. 

''Nimemefanya ziara ya kuzunguka maeneo ya huduma za usafiri kwa majini jijini Mwanza   nimefurahishwa na ninawapongeza kwa  juhudi mnazoonyesha kukidhi matakwa ya miongozo ya kazi zenu." Amesema Bwn. Mohamed.

Miongoni mwa wamiliki na waendeshaji wa vyombo walioshiriki kikao hicho ni pamoja na Kampuni ya Huduma za Meli Tanzania ( MSCL) ambayo Makao Makuu yake  ni jijini Mwanza, Mkombozi  fishing and Marine time transport, Songoro Marine, Nyehunge pamoja na wadau wengine wakiwemo Manahodha wa Meli.

Aidha, Bwn. Mohamed amegusia suala la Meli ya MV. Clarias kwamba taarifa rasmi itatoka baada ya zoezi la kuipandisha katika Chelezo kukamilika. MV. Clarias ilionyesha dalili za kuzama katika bandari ya Mwanza Kaskazini  kwa kulalia upande mmoja Mei 19, 2024.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo