Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

MKURUGENZI MKUU TASAC AWASHUKURU WADAU SABA SABA

Imewekwa: 21 July, 2025
MKURUGENZI MKUU TASAC AWASHUKURU WADAU SABA SABA

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Bw. Mohamed Salum amewashukuru wadau wanaoendelea kujitokeza kutembelea jengo la TASAC katika Maonesho ya Kimataifa Biashara Sabasaba yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere jijini Dar es Salaam.

Bw. Salum ametoa shukrani hizo leo tarehe 7 Julai, 2025 alipotembelea maonesho hayo.

"Nawashukuru wadau wote wanaotembelea Jengo la TASAC katika maonesho haya na natoa wito kwa wananchi na wadau wote kufika  hapa na kujifunza masuala mbalimbali kuhusu TASAC ikiwa ni pamoja na kujua fursa zilizopo katika sekta ya uchukuzi kwa njia ya maji," amesema Bw. Salum.

Aidha, Bw. Salum amepata fursa ya kutembelea wadau mbalimbali wa sekta ya usafiri nchini ikiwemo Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Kampuni ya Meli Tanzania (TASHICO), Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), Chuo cha Taifa cha Usafiri (NIT), pamoja na Mamlaka ya Usafiri Ardhini (LATRA).
 
Maonesho ya Sabasaba yaliyoanza tarehe 28 Juni, 2025 yanatarajia kufika kilele tarehe 13 Julai, 2025.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo