MKURUGENZI MKUU TASAC AFANYA MAZUNGUMZO NA US COAST GUARD

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Bw. Mohamed M. Salum leo tarehe 24 Februari 2025 amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe maalum wa Kikosi cha Ulinzi wa Pwani ya Marekani (US Coast Guard) na Mwakilishi wa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania.
Katika mazungumzo hayo, pande hizo zimejadili namna ambavyo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyotekeleza Mkataba wa Kimataifa wa Ulinzi wa Meli na Bandari (ISPS Code) pamoja na tishio jipya la uhalifu wa kimtandao. Ambapo ujumbe huo umeahidi kushirikiana na TASAC katika kutoa mafunzo ya kukabiliana na uhalifu wa kimtandao.
Ujumbe huo umeridhishwa na kupongeza namna ambavyo TASAC inatekeleza jukumu la usimamizi wa usalama wa meli na bandari kwa kufuata miongozo inayoendana na matakwa ya kimataifa.
Ujumbe huo unategemea kutembelea ya Bandari za Dar es Salaam na Malindi, Zanzibar ili kujionea namna zinavyotekeleza Mkataba wa ISPS Code.
Katika mkutano wawakilishi kutoka Mamlaka ya Bandari (TPA), DP World na Tanzania East Africa Gateway Terminal Limited (TEAGTL) walihudhuria mazungumzo hayo kwa mwaliko wa Mkurugenzi Mkuu.