MHE. RAIS DKT. SAMIA AZINDUA BANDARI KAVU NA TRENI YA MIZIGO YA SGR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amezindua Bandari Kavu ya Kwala pamoja na kuanza kwa safari za mizigo kwa kutumia treni ya SGR kuelekea Dodoma.
Hafla hii imefanyika leo, tarehe 31 Julai, 2025, na kuhudhuriwa na wananchi na viongozi mbalimbali.
Bandari hiyo ina uwezo wa kuhudumia makasha 823 kwa siku (takriban 300,000 kwa mwaka).
Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Prof. Makame Mbarawa amesema kuwa mchango wa sekta ya Uchukuzi kwenye pato la Taifa ni asilimia kati 14 hadi 16, kutokana na msukumo mkubwa Serikali ya Awamu ya Sita katika kuhakikisha kuwa sekta ya uchukuzi inachangia zaidi na kuongeza uwekezaji katika maeneo ya kimkakati.
Kwa upande wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) hafla hiyo ilihudhuriwa na Mwenyekiti wa Bodi wa TASAC, Naho. Mussa Mandia, Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Bw. Mohamed Salum pamoja na viongozi waandamizi wa Shirika.