Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

MHE. KIHENZILE AFUNGA RASMI MAADHIMISHO YA SIKU YA MABAHARIA DUNIANI

Imewekwa: 26 June, 2024
MHE. KIHENZILE AFUNGA RASMI MAADHIMISHO YA SIKU YA MABAHARIA DUNIANI

Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. David Mwakiposa Kihenzile amesema mabaharia wanatoa mchango wa asilimia 80 katika kukuza uchumi wa Tanzania.

Ameyasema hayo, wakati akiwa m
Mgeni rasmi kwa niaba ya Waziri wa Uchukuzi, Mhe.Prof.Makame Mbarawa wakati akifunga Maadhimisho ya Siku ya Mabaharia Duniani iliyohitimishwa leo tarehe 25 Juni, 2024 katika Viwanja vya Njia Njema wilayani Bagamoyo. 

Usafirishaji majini unasambaza bidhaa zenye gharama nafuu asilimia  90.  Mhe.David Kihenzile alisema "Serikali inawekeza kwenye vyombo  vya usafiri na miundombinu ya usafiri majini ili kukuza uchumi wa Tanzania na nchi jirani wanaotumia bandari ya Dar es salaam."

Aidha, Mkurugenzi Mkuu  wa TASAC, Bw. Mohamed Salum amesema siku hii ni kumbukizi ya mchango wa 
Mabahari katika kujenga uchumi wa Tanzania, kusoma tu  ni hatua ya kwanza ila lengo ni kupata ajira. 

"TASAC tunapambana kuingia makubaliano na Mataifa mengine ili Mabaharia wetu wapate ajira katika mataifa mbalimbali." Amesema Bw. Mohamed.

Mabaharia nao wameshukuru serikali na taasisi zake katika kusimamia maslahi yao na kuendelea kuboresha hali za mabaharia katika kufanya kazi na kupata haki zao.Hayo yamesemwa katibu Mkuu ZASU wakati akisoma riasala katika kilele cha maadhimisho siku ya mabaharia duniani na  kutambua mchango wa Serikali katika kuendeleza sekta ya Uchukuzi nchini.

Maadhimisho hayo yalianza tarehe 22 Juni, 2024 na kufungwa rasmi tarehe 25 Juni, 2024 yakiwa na kauli  mbiu Uendeshaji wa vyombo vya Usafiri Majini kwa siku za usoni: Usalama kwanza.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo