Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

Mhe. David Kihenzile afungua Semina ya Kikanda  wa Usalama wa Vyombo vya Usafiri kwa Njia ya Maji (AAMA)

Imewekwa: 23 April, 2024
Mhe. David Kihenzile afungua Semina ya Kikanda  wa Usalama wa Vyombo vya Usafiri kwa Njia ya Maji (AAMA)

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ipo tayari kuendelea kutoa ushirikiano kwa wadau wa sekta ya Usafiri kwa njia ya maji ili kuhakikisha usafiri unakuwa wa  usalama. 

 
Hayo yameelezwa na Naibu waziri Wizara ya Uchukuzi Mhe. David Kihenzile wakati akifunga Semina ya Kikanda  wa Usalama wa vyombo vya Usafiri kwa njia ya maji iliyofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwl. Julius Nyerere leo tarehe 17 Aprili, 2024 jijini Dar es Salaam.
 
 "Tanzania imekuwa mwanachama wa Shirika la Bahari Duniani (IMO) kwa takribani miaka 50 sasa na kumekuwa na juhudi za uboreshaji wa Sera ya Taifa ya Usafiri kwa njia ya maji unaoendelea nchini ni ishara tosha ya dhamira ya serikali kuboresha usalama wa usafiri kwa njia ya maji" amesema Kihenzile. 
 
Aidha, Waziri Kihenzile amewakaribisha wageni mbalimbali waliohudhuria mkutano huo kutenga muda wa kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini kwani Tanzania ni nchi inayoongoza barani Afrika kwa kuwa na vivutio vingi vya utalii na ikishika nafasi ya pili ulimwenguni. 
 
Kwa upande wake Muwakilishi wa Mkurugenzi wa IMO Bw. Vicent Job ameiomba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufanyia kazi mambo mbalimbali yaliyojadiliwa katika mkutano huo ili kuboresha usalama wa usafiri kwa njia ya maji huku akitoa shukurani  kwa ukarimu na kukubali kuwa mwenyeji wa Mkutano huo.

Mkurugenzi wa Usalama na Mazingira Wizara ya Uchukuzi Stella Katondo amewashukuru washiriki kwa kuhudhuria mkutano huo huku akiwaasa washiriki kutekeleza maazimio yaliyofikiwa katika mkutano huo ili kuimarisha usalama wa usafiri kwa njia ya maji.

Semina hiyo ya siku mbili ya tarehe 16 na 17 Aprili, 2024 ilihudhuriwa na nchi mbali mbali za ndani na nje ya Afrika ikiwemo Uingereza, Sweden, China, Marekani, Ujerumani, Uholanzi na Canada, Nigeria, Kenya, Uganda, Senegal, Gabon, DRC, Afrika Kusini, Togo, Cameroon na  Carpeverde.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo