Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

Mhe. Atupele Mwakibete ( MB), Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi azindua ripoti ya sensa ya Vyombo Vidogo vya Usafiri Majini iliyofanywa na TASAC kwa kushirikiana na NBS

Imewekwa: 14 July, 2023
Mhe. Atupele Mwakibete ( MB), Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi azindua ripoti ya sensa ya Vyombo Vidogo vya Usafiri Majini iliyofanywa na TASAC kwa kushirikiana  na NBS

Mhe. Atupele Mwakibete ( MB), Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi amezindua ripoti ya sensa ya vyombo vidogo vya usafiri Majini iliyofanya na Shirika 
 la  Uwakala wa Meli Tanzania- TASAC kwa kushirikiana  na ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).  

Ripoti hiyo ya sensa inayotajwa kuwa ni sensa ya kwanza kuwahi kufanyika nchini, imezinduliwa tarehe 11 Julai, 2023 katika ukumbi wa mikutano Anatoglo,  Jijini Dar es Salaam.
  
 Mhe. Mwakibete ameeleza kuwa  ripoti hiyo itasaidia kuboresha sera na kutaja fursa zilizopo katika kukuza uchumi wa Taifa na watu wake kupitia uchumi wa buluu unaoenda sambamba na ukuaji wa sekta ya usafiri majini kwa vyombo vidogo katika mito, mabwawa, maziwa na hata bahari.

 Aidha naibu Waziri Mwakibete amewataka wadau mbalimbali kutumia taarifa  hiyo kibiashara kwa kuangazia maeneo yenye vyombo vingi vya usafiri wa majini ili kufungua biashara za uuzaji wa vipuri vya boti,maboya,injini na vifaa vingine.

"kwa mujibu wa taarifa ya sensa jumla ya idadi ya vyombo vidogo vya majini ni 52,189, pia kuna jumla ya mialo 885,idadi ya vyombo vidogo vya majini vyenye urefu wa mita nne au zaidi kwenye maeneo ya maji ni 45,976,kati ya hivyo Asilimia 53.65% vipo Ziwa Victoria, 13.41% vipo Bahari ya Hindi,10.28% vipo Ziwa Tanganyika,7.65 vipo Ziwa Nyasa na Asilimia 15.1% vipo katika maeneo mengine ya maziwa na mabwawa nchini" Amesema Mwakibete .

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa  TASAC, Bw.  Kaimu Abdi Mkeyenge amesema wakati wa  uandaaji wa sensa hiyo wameshirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS),Wizara ya ujenzi na uchukuzi,TAMISEMI , Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya Uchukuzi.
“Baada ya kukamilika kwa sensa hii,tumeweza kuunda kanzi data maalumu inayorahisisha kuvitambua vyombo hivyo,wamiliki na maeneo vilipo na kurahisisha utambuzi wa vyombo na hali yake na endapo kikitapata majanga kuweza kukifikia kwa haraka na kutambua ni chombo kipi kimehusika kwenye ajali au changamoto yoyote majini” Amesema Mkurugenzi Mkuu huyo wa TASAC Kaim Mkeyenge. 

 Ofisi ya Taifa ya Takwimu imesema ni mara ya kwanza NBS imeshiriki katika sensa ya vyombo vya majini na kuipongeza TASAC kwa hatua hiyo na kuongeza kuwa kanzi data iliyoundwa itasaidia sana Wafanyabiashara,wadadisi na watafiti mbalimbali kufanyakazi yao kwa urahisi zaidi.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo