Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

Mabaharia watoa elimu kwa vitendo namna ya kumwokoa mtu aliyeangukakwenye Maji.

Imewekwa: 25 June, 2023
Mabaharia watoa elimu kwa vitendo namna ya kumwokoa mtu aliyeangukakwenye Maji.

Katika kuadhimisha Siku ya Mabaharia Dunia, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa kushirikiana na wadau wa usafiri majini Nchini wameendelea kutoa elimu ya usafiri salama majini kwa kuonyesha kwa vitendo namna ya kumwokoa mtu aliyetumbukia majini.

Zoezi hilo limefanyika Jumamosi tarehe 24/6/2023 katika eneo la Ziwa Victoria pembezoni mwa kisiwa kidogo cha Richard huku Mkurugenzi wa Usalama wa Usafiri na Utunzaji wa Mazingira Bi.Stella Katondo, Mkuu wa chuo cha Bahari Cha Dares salaam Dkt.Tumaini Gulumo na Meneja za Huduma za Ubaharia TASAC Bwana Lameck Sondo wakishuhudia zoezi hilo. 

Wananchi waliokuwa kwenye vivuko vinavyomilikiwa na Mkombozi na Kamanga waliweza kushudia kuona mfano wa abiria aliyejirusha majini na kuokolewa na vyombo vya Serikali na kumpatia huduma ya kwanza.

Zoezi hilo lilifanywa na mabaharia pamoja na wataalam kwa ushirikiano wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi -SMZ, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Mamlaka ya Usafiri wa Bahari Zanzibar (ZMA), Jeshi la Polisi wanamaji, Kikosi cha Kuzuia Magendo, Shirika la Meli Zanzibar, Chuo cha Bahari Dar es salaam, DANAOS, Chama cha Mabaharia Tanzania (TASU), Chama cha Mabaharia Zanzibar na Kampuni ya Huduma za Meli Tanzania (MSCL).

Mrejesho, Malalamiko au Wazo