Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

Kushiriki michezo ni kujenga afya kazini na nyumbani

Imewekwa: 18 January, 2024
Kushiriki michezo ni kujenga afya kazini na nyumbani

Kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala Bw. Issa Chande kutoka Wizara ya Uchukuzi amehimiza wafanyakazi wa serikali kushiriki bonanza na mazoezi ili kujenga afya zao katika Bonanza la Uchukuzi lililofanyika Viwanja vya TCC Chang'ombe tarehe 16 Disemba, 2023 jijini Dar es Salaam.

 "Mnapocheza mchezo wa kuvuta kamba, kukimbia, kupiga mpira na kucheza michezo ya jadi inasaidia kuburudisha akili na kujenga afya ya akili, misuli na mfumo wa upumuaji. Pia mkishiriki michezo na mazoezi huimalisha afya kazini na nyumbani". Amesema Bw. Chande.

Kwa upande wa  Mkurugenzi Mkuu wa LATRA CPA. Habibu Suluo kwa niaba ya Wakurugenzi wakuu wa taasisi zilizochini ya Wizara ya Uchukuzi amesema anashukuru timu ya uchukuzi kwa kuunganisha wafanyakazi na menejimeti kutoka Wizara ya Uchukuzi, TASAC, LATRA, TCAA, TAA, TPA, Chuo cha Bahari Dar es salaam - DMI, TRC, TAZARA, TMA, ATCL na Shirika Huduma za Meli Tanzania. 

Aidha, Mkurugenzi wa Huduma za Shirika TASAC, Bw. Hamidu Mbegu aliyekuwa mlezi wa timu ya uchukuzi kwa miaka 5 amesema ushirikiano daima ndio siri ya
mafanikio ya timu.

"Hata kama sasa ni Mkurugenzi wa Huduma za Shirika TASAC  nitaendelea kuwapa ushirikiano mara utakapohitajika" Amesema Bw. Mbegu.

Michezo imekuwa ni sehemu ya kujenga ushirikiano wa taasisi na taasisi, wafanyakazi wa ngazi za chini na menejimenti za taasisi mbalimbali na hata jamii ya Watanzania.

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limeshiriki kikamilifu kwa kucheza michezo ya mpira kwa kuunda timu ya ushirikiano kati ya TASAC, Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Nchi Kavu (LATRA), Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT) dhidi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuvuta kamba na michezo ya jadi.

Katika bonanza hilo TPA walikuwa kinara kwa kuchukuwa makombe 4 kati ya makombe 6 yaliyoshindaniwa.

Bonanza hili la tatu kufanyika mwaka huu, bonanza la kwanza lilifanyika Januari na liliandaliwa na LATRA, bonanza la pili lilifanyika Juni na liliandaliwa na TASAC  na la tatu limeandaliwa na TPA.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo