Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi aongoza kikao kati ya Serikali na wadau wa usafirishaji kwa njia ya maji

Imewekwa: 22 May, 2024
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi aongoza kikao kati ya Serikali na wadau wa usafirishaji kwa njia ya maji

Prof Godius Kahyarara, Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi ameongoza kikao kati ya Serikali na wadau wa usafirishaji kwa njia ya maji na kujadiliana masuala mbalimbali yanayohusu Sekta hiyo hususan gharama za usafirishaji zilizoongezeka hivi karibuni katika bandari ya Dar es Salaam.
Kikao hiko chenye lengo la kutatua changamoto mbalimbali kimefanyika katika ukumbi wa LATRA jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka taasisi binafsi na za Umma zikiwemo Shirika la Uwakala wa Meli (TASAC), TRA na TPA.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo