Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

KATIBU MKUU UCHUKUZI ATETA NA MKURUGENZI MKUU TASAC

Imewekwa: 26 February, 2025
KATIBU MKUU UCHUKUZI ATETA NA MKURUGENZI MKUU TASAC

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara ameteta na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Bw. Mohamed Salum, leo tarehe 26 Februari 2025 wakati wa ziara ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania wilayani Pangani mkoani Tanga.

Moja ya masuala waliyozungumza ni kuhusu usalama wa usafiri majini mkoani Tanga na hasa katika wilaya ya Pangani na mkoa wa Tanga kwa ujumla pamoja na maendeleo ya miundombinu ya sekta ya huduma za uchukuzi kwa ajili ya maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi nchini.

Katika ziara hiyo Mheshimiwa Rais amezindua boti zaidi ya 30 za uvuvi kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Daraja la Mto Pangani na ambapo alisisitiza kuwa daraja hilo litakua kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi mkoani Tanga.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo