Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

KAMATI YA PAC BARAZA LA WAWAKILISHI YAFANYA ZIARA YA MAFUNZO TASAC

Imewekwa: 12 October, 2024
KAMATI YA PAC BARAZA LA WAWAKILISHI YAFANYA ZIARA YA MAFUNZO TASAC

Wajumbe wa Kamati ya Baraza la Wawakilishi ya Hesabu za Serikali (PAC) - Zanzibar na watendaji wa Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA) wamefanya ziara ya mafunzo katika Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) leo tarehe 10 Oktoba, 2024.

Ugeni huo uliongozwa na Mweyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Mwanaidi Kassim Mussa.

Lengo la ziara hiyo ni kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na TASAC kwa kuzingatia kanuni, taratibu na Sheria za Usafiri Majini na ya Uwakala wa Meli Tanzania Sura 415.

Mkurugenzi wa Huduma za Shirika (TASAC), Bw. Hamid Mbegu ambaye amemuwakilisha Mkurugenzi Mkuu amewashukuru wajumbe wa Baraza hilo kwa kuchagua kujifunza kutoka kwa TASAC namna mbalimbali wanavyoendesha shughuli za utendaji za Shirika.

“Tunajivunia ujio wenu wenye lengo la kujifunza katika Shirika letu kwani imeonesha ni kwa namna gani mnatuthamini, lakini pia mnakithamini kile tunachokifanya, tunawaahidi kudumisha mashirikiano baina yetu kwa manufaa ya Taasisi zetu pamoja na Watanzania kwa ujumla,” amesema Bw. Mbegu.

Aidha, wajumbe hao wamepta nafasi ya kutembelea Kituo cha Uratibu, Utafutaji na Uokoaji (MRCC) kilichopo Dar es Salaam kinachosimamiwa na TASAC kupitia Kurugenzi ya Usalama, Ulinzi wa Usafiri Majini na Utunzaji wa Mazingira pamoja na Mamlaka ya Usimamizi wa  Bandari Tanzania (TPA).

Mrejesho, Malalamiko au Wazo