Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Bw. Nelson Mlali amewatunuku vyeti wahitimu 198 wa kidato cha Nne katika shule ya Sekondari Goba leo tarehe 19 Oktoba, 2023.

Imewekwa: 27 October, 2023
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Bw. Nelson Mlali amewatunuku vyeti wahitimu 198 wa kidato cha Nne katika shule ya Sekondari Goba leo tarehe 19 Oktoba, 2023.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Bw. Nelson Mlali amewatunuku vyeti wahitimu 198 wa kidato cha Nne katika shule ya Sekondari Goba leo tarehe 19 Oktoba, 2023.

Akizungumza katika mahafali hayo Bw. Mlali amefurahishwa sana kuona kuwa Shule hiyo inaendelea kujitahidi kuimarisha mazingira ya kufundishia na kujifunzia, hii inaonesha dhamira ya dhati ya kuendelea kuboresha elimu kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Bw. Mlali ameongeza kwa kusema “Hii ni siku yenu, siku ya kujivunia kazi ngumu mliyoifanya kwa miaka hii yote. Hongereni sana. Ninaamini kuwa elimu ndiyo ufunguo wa maendeleo na mabadiliko katika jamii. Wanafunzi mnayo nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko chanya katika jamii yetu. Ni matumaini yangu kuwa mtatumia elimu mliyoipata hapa kuwa raia wema na kuchangia katika maendeleo ya nchi yetu."

Aidha, amewapongeza walimu kwa jukumu kubwa wanalolifanya katika kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora.

 “Walimu, mmekuwa nguzo muhimu katika safari ya elimu ya wanafunzi hawa, kwa kujitolea kwa moyo wote katika kuwafundisha, kuwaongoza, na kuwajenga kiakili”. Alisema Bw. Mlali.

Mahafali hayo yamefanyika katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Goba jijini Dar es Salaam.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo