Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

IOMOU YASHEREHEKEA MIAKA 25 YA UTEKELEZAJI WAKE

Imewekwa: 09 September, 2024
IOMOU YASHEREHEKEA MIAKA 25 YA UTEKELEZAJI WAKE

Nchi wanachama wa Hati ya Makubaliano ya Ukaguzi wa Meli katika Bahari ya Hindi (IOMOU) wameshereheka Miaka 25 tangu kuanza utekelezaji wa Hati hiyo mwaka 1999.

 

Akizungumza wakati wa ghafla fupi ya kusherehekea maadhimisho hayo Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira, Wizara ya Uchukuzi, Bi. Stella Katondo amesema anawapongeza nchi wanachama wote kwa kufikia miaka 24 katika kutekeleza hati hiyo kwa kipindi cha miaka 25 na akaongeza kuwa ni ushahidi tosha wa namna ambavyo nchi zinajitolea kusimamia usalama, ulinzi na utunzaji wa mazingira ya bahari.

 

“Katika miaka hii 25, IOMOU imekuwa kinara wa kusimamia ushirikiano wa kikanda na kutoa miongozo na kuhakikisha Bahari zinakuwa salama ama kwa hakika huu ni upendeleo wa hali ya juu” amesema Bi. Katondo.

 

Aidha, amesema kuwa ni muhimu kukumbuka kuwa sherehe hizi si tu zinatoa fursa ya kutafakari juu ya mafanikio ya zamani lakini pia kuendeleza ushirikiano huu muhimu kwa maendeleo ya baadaye.

 

Naye Katibu wa IOMOU, Bw. Achintya Dutta ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Uchukuzi na TASAC kwa kukubali kuwa mwenyeji wa Mkutano huu pamoja na kufanya sherehe fupi ya kuadhimisha Miaka 25 ya utekelezaji wa IOMOU.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo