Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

IMO-YAIJENGEA UWEZO KAMATI YA USALAMA YA USAFIRI MAJINI TANZANIA

Imewekwa: 07 August, 2025
IMO-YAIJENGEA UWEZO KAMATI YA USALAMA YA USAFIRI MAJINI TANZANIA

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Bw. Mohammed Salum,  amesema ni muhimu kuimarisha usalama na kulinda  usafiri majini katika maeneo ya Bahari dhidi ya changamoto mbalimbali zinazojitokeza. 

Amesema hayo leo tarehe 28 Julai, 2025 katika Ukumbi wa Mikutano wa hoteli ya "Four Point" ya jijini Dar Es Salaam, wakati akifungua warsha ya Mazoezi ya Mezani ya Kamati ya Kitaifa ya Usalama wa Baharini.

Akizungumza katika uzinduzi huo Bw. Salum amesema usafiri majini ni muhimu kwa maendeleo ya taifa letu kwa sababu asilimia 90 ya mizigo tunayotumia inasafirishwa kwa njia ya maji. Hivyo, ni muhimu kuwa na uelewa wa pamoja wa kutathmini maandalizi yetu dhidi ya vitisho mbalimbali vya usalama majini, na hatimaye kukuza mikakati ya usalama kwa ngazi ya kitaifa.

"Leo tunaanza Zoezi letu la kwanza la Meza ya Kitaifa la mkakati wa usalama wa majini, tunalenga kujiweka tayari kukabiriana na changamoto ya usalama wa majini. Sote tunatambua umuhimu wa kulinda maeneo yetu ya baharini na kujiweka tayari", amesema Bwana Salum.

Ameongeza kuwa "Nafasi ya Tanzania katika bahari na ushiriki wake hai ndani ya Shirika la Bahari Duniani -IMO unaiweka nchi kuwa  muhimu katika masuala ya bahari Kitaifa na Kimataifa. Tushirikiane kushughulikia vitisho vya sasa vya usalama wa majini na kuendeleza hatua endelevu za usalama na utekelezaji wake katika viwango vya Kitaifa na Kimataifa. Kwa pamoja, tunaweza kuhakikisha ukuaji endelevu wa sekta yetu ya usafiri majini na Uchumi wa Buluu." Amesema Bwana Salim.

Warsha hiyo imeanza leo tarehe 28 hadi tarehe 30, Julai, 2025 na taasisi mbalimbali za Tanzania zinashiriki ikiwemo, Wizara ya Uchukuzi, Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Polisi, Mamlaka ya Bandari Tanzania, Mamlaka ya Usafiri wa Bahari Zanzibar na wengineo.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo