GAWIO DAY: TASAC YAKABIDHI HUNDI YA SHILINGI BILIONI 16.3

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), leo Jumanne, Juni 10, 2025, limemkabidhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, mfano wa hundi yenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 16.3 ikiwa ni asilimia 15 ya mapato ghafi kutoka TASAC kwa mwaka wa fedha 2024/25.
Hundi hiyo imekabidhiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya TASAC, Nahodha Mussa Mandia katika hafla ya kupokea gawio na michango kutoka kwa taasisi na mashirika ya umma iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Pichani, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Mwenyekiti wa Bodi ya TASAC, Nahodha Mussa Mandia na Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Bw. Mohamed Salum.