Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

DG TASAC AWAHIMIZA WATUMISHI KUZINGATIA WELEDI

Imewekwa: 04 November, 2024
DG TASAC AWAHIMIZA WATUMISHI KUZINGATIA WELEDI

Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Bw. Mohamed Salum amewahimiza watumishi wa Shirika kuwa weledi na kutoa huduma bora kwa wateja ili kufikia malengo ya kuanzishwa kwake.

 

Bw. Salum ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa wafanyakazi wa TASAC, leo tarehe 01 Novemba, 2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere, mjini Kibaha, mkoani Pwani.

 

Bw. Salum amesema kuwa watumishi wanapaswa kuwa weledi ili kuchagiza ukuaji wa Sekta ndogo ya usafiri majini kwa kuzingatia Sheria,kanuni na taratibu za utumishi wa umma, na hivyo kujipanga vema katika kutumia rasilimali watu ili kusaidia maendeleo ya sekta ya usafiri majini.

 

"Sisi kama watumishi wa umma utendaji wetu unaongozwa na Sheria, Kanuni na taratibu za utumishi wa umma, hivyo, ushirikiano na mahusiano mazuri mahala pa kazi ni muhimu katika utekelezaji wa majukumu yetu ya kila siku na kusaidia taasisi yetu kuwa shindani kikanda na duniani,” amesema Bw. Salum.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo