TAARIFA KWA UMMA ZUIO LA MITUMBWI/ FIBRE KUFANYA BIASHARA YA KUBEBA ABIRIA WILAYA YA KIGAMBONI

Imewekwa: Jul 08, 2022


TAARIFA KWA UMMA

ZUIO LA MITUMBWI/ FIBRE KUFANYA BIASHARA YA KUBEBA ABIRIA WILAYA YA KIGAMBONI

Kutokana na changamoto ya ubovu wa kivuko cha MV Kazi ambacho kipo kwenye matengenezo kwa sasa, vivuko vinavyosafirisha abiria kati ya eneo la Feri na Kigamboni havikidhi mahitaji kutokana na idadi kubwa ya abiria wanaotumia vivuko hivyo. Hali hii imepelekea mitumbwi ya uvuvi maarufu kama Fiber kuanza kufanya biashara ya kubeba abiria kinyume cha sheria.

Ni ukiukwaji wa masharti ya usalama na uendeshaji kwa Mmiliki au Mwendesha chombo popote nchini kutumia chombo kinyume na makusudio yaliyoainishwa kwenye cheti cha ubora na leseni iliyotolewa na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC). Hivyo, hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wote wanaotumia mitumbwi/ fibre kubeba abiria wakati zina leseni za kufanya shughuli za uvuvi kwa kuwa wanafanya biashara hatarishi. Wananchi wanaombwa kutoa taarifa za ukiukwaji wa usalama wa uendeshwaji wa vyombo vya usalama majini kwa TASAC kupitia simu za bure: 0800110101 na 0800110107, barua pepe: info@tasac.go.tz au kufika katika ofisi ya TASAC iliyo karibu.

Aidha, tatizo la upungufu wa vivuko tayari limeshughulikiwa na Serikali kwa kuingia kwenye makubaliano na Kampuni ya Azam Marine ambapo boti zake mbili sasa zinatoa huduma ya kuvusha abiria kati ya Feri na Kigamboni.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu

SHIRIKA LA UWAKALA WA MELI TANZANIA

4 Julai, 2022