TANZIA

Imewekwa: May 12, 2020


TANZIA

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), kwa masikitiko makubwa anatangaza kifo cha Mkurugenzi wa Ulinzi, Usalama wa Vyombo vya Usafiri Majini na Utunzaji wa Mazingira ya Bahari (DMSE) Mhandisi Japhet L. Loisimaye kilichotokea tarehe 10 Mei, 2020 jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu anatoa pole kwa familia, wafanyakazi na wote walioguswa na msiba huu.

Hakika atakumbukwa kwa uchapakazi, uadilifu na uzalendo katika kipindi chake chote cha uhai wake.

Tunawaombea wote faraja na subira njema katika kipindi hiki kigumu cha majonzi. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.

AMIN

Imetolewa na;

MKURUGENZI MKUU

SHIRIKA LA UWAKALA WA MELI TANZANIA (TASAC).