Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

WADAU MBALIMBALI WAPATIWA ELIMU YA USAFIRI MAJINI NANENANE - DODOMA

Imewekwa: 03 August, 2026
WADAU MBALIMBALI WAPATIWA ELIMU YA USAFIRI MAJINI NANENANE - DODOMA

Wadau mbalimbali wametembelea Banda la Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo NaneNane yalifunguliwa rasmi leo tarehe 1 Agosti, 2026 katika Viwanja vya John Samuel Malecela, Nzuguni jijini Dodoma.

 

Katika banda la TASAC wadau hao wamepatiwa elimu kuhusu majukumu ya shirika, umuhimu wa kuzingatia sheria na kanuni za usafiri majini, matumizi sahihi ya vifaa vya kuokoa maisha, pamoja na hatua zinazochukuliwa na TASAC kuhakikisha usafiri majini unakuwa salama, wenye ufanisi na unaolinda mazingira.

 

Aidha, wadau hao wamepata fursa ya kuuliza maswali na kupata ufafanuzi kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na TASAC, ikiwemo usajili na ukaguzi wa vyombo vya majini, utoaji wa leseni kwa mabaharia na hatua za kuimarisha usalama katika sekta ya usafiri majini nchini.

 

Wananchi waliotembelea banda hilo wameeleza kuridhishwa na elimu wanayoipata, wakisema imewaongezea uelewa kuhusu wajibu wa kila mdau katika kuhakikisha usalama wa usafiri majini na umuhimu wa kufuata taratibu zilizowekwa.

 

Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo NaneNane ya mwaka 2026 yanaongozwa na kaulimbiu isemayo, “Tambua Soko; Ongeza Tija Kutekeleza Dira 2050,” yakikusanya taasisi mbalimbali za umma na binafsi zinazowasilisha huduma, teknolojia na ubunifu kwa wananchi.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo