TASAC MKOANI GEITA YATOA TAHADHARI DHIDI YA EL NINO KWA WADAU WA USAFIRI MAJINI
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kupitia Ofisi ya Mkoa wa Gita imewaasa wadau wa usafiri majini Mkoani Geita kuchukua tahadhari dhidi ya El Nino inayotarajiwa kuathiri msimu wa mvua za Vuli 2026, hii ni kutokana na taarifa rasmi iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Afisa Mfawidhi Mkoa wa Geita (OIC) wa TASAC, Nahodha Gogfrey Chegere, wakati wa semina ya utoaji elimu kuhusu kuchukua tahadhari dhidi ya athari zinazoweza kujitokeza kutokana na hali ya hewa ya El Nino katika mialo mbalimbali Mkoani Geita.
Nahodha Chegere amesema kuwa ili kujihadhari na mvua hizo za El Nino ni wajibu wa kila mmiliki na mtumiaji wa chombo cha majini kuhakikisha chombo chake kinakuwa na vifaa vyote muhimu vya usalama kabla ya kuanza safari hususan jaketi okozi, pamoja na kuhakikisha vinatumika ipasavyo.
‘’Ni muhimu kwa kila anayefanya kazi katika chombo kuhakikisha kimesajiliwa na TASAC na kina cheti halali ambacho hakijaisha muda wake vilevile chombo kiwe na jaketi okozi za kutosha na watumiaji wazivae wakati wote wanapokuwa safarini,” alisema Nahodha. Chegere.
Dhumuni la utoaji elimu huu ni kuwaasa kuwasihi kuchukua tahadhari kutokana na kukabiliana na mvua kubwa inayoweza kusababisaha upepo mkali. Hata hivyo TASAC inawaasa wananchi na wadau wa usafiri majini kufuatilia taarifa rasmi za hali ya hewa kabla na wakati wa safari na kuzingatia maelekezo ya usalama na epuka kusafiri wakati hali ya hewa si salama.