TASAC YAANZA RASMI MAFUNZO YA MFUMO MPYA WA MTRS
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Agosti 12, 2026 limeanza rasmi mafunzo kwa watoa huduma za usafiri wa majini kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa kielektroniki wa Maritime Transport e-Regulatory System (MTRS).
Mafunzo hayo yanafanyika katika ukumbi wa Garden Avenue (PPF TOWER), jijini Dar es Salaam, yakilenga kuwaandaa watoa huduma kabla ya mfumo huo kuanza kutumika rasmi Septemba 2026.
Mfumo wa MTRS umeunganishwa na mifumo mingine ya Serikali, ikiwemo TRA na BRELA, ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa njia ya kielektroniki.
Kupitia mfumo huo, watumiaji wataweza kujisajili, kupata ankara za malipo, kufanya malipo na kuchapisha vyeti pamoja na taarifa nyingine muhimu kwa njia ya kielektroniki.
Mafunzo hayo yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 28 Agosti, 2026.