Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

MSAJILI WA MABAHARIA AKABIDHI RAMBIRAMBI YA JUMUIYA YA MABAHARIA KWA FAMILIA YA BAHARIA MONGU

Imewekwa: 01 July, 2026
MSAJILI WA MABAHARIA AKABIDHI RAMBIRAMBI YA JUMUIYA YA MABAHARIA KWA FAMILIA YA BAHARIA MONGU

Msajili wa Mabaharia nchini, Bw. Mohamed Salum, amekabidhi rambirambi zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 3 zilizotolewa na Jumuiya ya Mabaharia nchini Tanzania kwa familia ya marehemu Nahodha Mchama Maregesi Mongu, baharia wa Kitanzania aliyefariki dunia tarehe 3 Mei 2026 akiwa kazini ndani ya meli ya kuvuta (tug boat) katika Mfereji wa Hormuz.

Akikabidhi rambirambi hizo, Bw. Salum alisema mchango huo unaakisi mshikamano na moyo wa kujali uliooneshwa na jumuiya ya mabaharia nchini kwa familia ya marehemu katika kipindi hicho kigumu cha maombolezo. 

Aliongeza kuwa TASAC itaendelea kusimamia ustawi, haki na maslahi ya mabaharia wa Kitanzania, wakiwa nchini na wanapotekeleza majukumu yao katika meli zinazofanya kazi nje ya nchi.

Rambirambi hizo zilipokelewa kwa niaba ya familia na kaka wa marehemu, Bw. Cyprian Majembe, ambaye aliishukuru Jumuiya ya Mabaharia nchini Tanzania pamoja na Msajili wa Mabaharia kwa kuwafariji na kuonesha mshikamano katika kipindi hicho kigumu. Alisema faraja na msaada huo umeipa familia nguvu ya kuendelea kuvumilia msiba huo.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo