Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

MKOA WA MWANZA WAASWA KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA EL NINO

Imewekwa: 22 September, 2026
MKOA WA MWANZA WAASWA KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA EL NINO

Wadau wa usafiri majini Mkoa wa Mwanza wametakiwa kuchukua tahadhari na kuzingatia hatua za usalama kutokana na utabiri wa hali ya hewa unaoashiria uwepo wa El Nino katika msimu wa mvua za Vuli 2026, kwa mujibu wa taarifa rasmi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).

Hayo yamezungumzwa na Afisa Mfawidhi (OIC) wa ofisi yaTASAC Mkoa wa Mwanza, Nahodha Paul Msokwa, wakati wa semina ya kutoa elimu kuhusu namna ya kujikinga na athari zinazoweza kusababishwa na hali hiyo ya hewa. 

Akizungumza katika semina hiyo, Naho. Msokwa amewasisitiza wadau kuchukua tahadhari wawapo majini ilikuepuka changamoto yoyote inayoweza kotokea kutokana na mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha.  

‘’Nawasihi wamiliki na watumiaji wa vyombo vya usafiri majini kuhakikisha vyombo vyao vinakuwa na vifaa muhimu vya usalama kabla ya kuanza safari, hususan jaketi za kuokoa maisha, na kuhakikisha zinatumika ipasavyo wakati wote wa safari’’, amesema Msokwa

Aidha, amewataka wadau kuhakikisha vyombo vyao vimesajiliwa na TASAC na vina vyeti halali, pamoja na kuwa na idadi ya kutosha ya jaketi za kuokoa maisha kwa ajili ya watumiaji wote.

Wananchi na wadau wa usafiri majinikufuatilia taarifa rasmi za hali ya hewa kabla na wakati wa safari, kuzingatia maelekezo ya usalama na kuepuka kusafiri endapo hali ya hewa si salama.

 “Usalama wako na wa abiria ni jukumu letu sote. Kila mmoja wetu hana budi kuchukua tahadhari.”

Mrejesho, Malalamiko au Wazo