Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

KAMATI YA MIUNDOMBINU, ARDHI NA TEHAMA YA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR YATEMBELEA BANDA LA TASAC NANENANE

Imewekwa: 05 August, 2026
KAMATI YA MIUNDOMBINU, ARDHI NA TEHAMA YA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR YATEMBELEA BANDA LA TASAC NANENANE

Kamati ya Miundombinu, Ardhi na TEHAMA ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, leo tarehe 4 Agosti 2026, imetembelea Banda la Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. John Malecela, Nzuguni, jijini Dodoma.

Wakati wa ziara hiyo, wajumbe wa Kamati wamepewa maelezo kuhusu majukumu ya TASAC katika kusimamia usalama, ulinzi na utunzaji wa mazingira katika sekta ya usafiri majini. Aidha, wameelezwa kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na Shirika katika kusimamia sekta ya usafiri kwa njia ya maji.

Wajumbe wamepata fursa ya kujifunza zaidi kuhusu mchango wa TASAC katika kuhakikisha usafiri salama na endelevu majini, pamoja na jitihada za Shirika za kutoa elimu kwa umma kuhusu uzingatiaji wa sheria, kanuni na taratibu za usafiri majini.

Maonesho hayo yanaongozwa na kaulimbiu isemayo, “Tambua Soko; Ongeza Tija Kutekeleza Dira 2050,” yanaendelea hadi tarehe 8 Agosti 2026. 

TASAC inawakaribisha wananchi, wadau wa sekta ya usafiri majini na washiriki wote kutembelea Banda lake lililopo ‘Government Pavilion 3’, ili kujifunza zaidi kuhusu majukumu na huduma zinazotolewa na Shirika, pamoja na kupata elimu kuhusu usalama, ulinzi na utunzaji wa mazingira katika usafiri majini.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo