Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi (SMZ) Mhe. Khalid Salum ametoa rai kwa wananchi kuzingatia umuhimu wa bahari kwa kutumia njia sahihi za kuvuna rasilimali za bahari.

Imewekwa: 07 October, 2023

Mhe. Salum ameyasema hayo katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani 2023 yaliyofanyika katika viwanja vya Gombani Nje visiwani Pemba - Zanzibar tarehe 28 Septemba, 2023.

"Tunavua samaki, tunasafiri, tunafanya utalii kwenye fukwe, tunajiajiri na kuajiriwa lakini pia asilimia 50 ya hewa tunayovuta ya oksijeni vyote hivyo vinatokana na bahari hivyo bahari ni maisha kwa jamii nzima, ni muhimu kuilinda na kuhifadhi mazingira ya bahari ili yaendelee kuwa salama kwa manufaa yetu na manufaa ya Taifa kwa ujumla". Amesema Mhe. Salum.

Aidha, Mhe. Salum amewapongeza TASAC na ZMA kwa kuwashirikisha wadau wa sekta nyingine ambao ni Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar (ZAA) na Mamlaka ya Udhibiti usafiri barabarani Zanzibar kwa kuadhimisha Siku ya Bahari Duniani.

Maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani 2023 yenye Kauli mbiu "Miaka 50 ya MARPOL, uwajibikaji wetu unaendelea" yalianza rasmi tarehe 25 Septemba, 2023 na kuhitimishwa leo tarehe 28 Septemba, 2023 katika viwanja vya Gombani Nje visiwani Pemba - Zanzibar.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo