Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

TASAC YASHIRIKI C-CEOs FORUM 2026 ARUSHA

Imewekwa: 30 September, 2026
TASAC YASHIRIKI C-CEOs FORUM 2026 ARUSHA

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limeshiriki katika *Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma (C-CEOs Forum) 2026, kinachofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), jijini Arusha.

Kikao hicho kilifunguliwa jana tarehe 28 Septemba, 2026 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, na kuwakutanisha Wenyeviti wa Bodi pamoja na Watendaji Wakuu wa taasisi na mashirika ya umma kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali yanayohusu ufanisi, usimamizi wa rasilimali na utendaji wa taasisi za umma.

Katika kikao hicho, Mhe. Ndejembi amesisitiza umuhimu wa Taasisi na Mashirika ya Umma kuimarisha usimamizi wa rasilimali, kuongeza ufanisi na kuhakikisha yanaendelea kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya Taifa.

Ushiriki wa TASAC katika C-CEOs Forum 2026 unaendelea kuonesha dhamira ya Shirika katika kujifunza na kubadilishana uzoefu na taasisi nyingine za umma, hususan katika maeneo ya utawala bora, uwajibikaji, ufanisi wa kiutendaji na utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Kikao hicho pia kimetoa fursa kwa viongozi wa taasisi na mashirika ya umma kujadili changamoto zinazokabili utekelezaji wa majukumu yao na kuweka mikakati ya kuimarisha utendaji, matumizi bora ya rasilimali na mchango wa taasisi katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Taifa.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo