TASAC YAENDELEA KUTOA MAFUNZO KUHUSU MFUMO MPYA WA MTRS
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) linaendelea kutoa mafunzo kwa wadau wa sekta ya usafiri majini kuhusu mfumo mpya wa kielektroniki wa Maritime Transport e-Regulatory System (MTRS). Mfumo huu unatarajiwa kuchukua nafasi ya mfumo wa sasa wa Manifest Billing System (MBILL).
Mfumo wa MTRS, unaotarajiwa kuanza kutumika mwezi Septemba 2026, unalenga kuongeza ufanisi na uwazi katika utoaji wa huduma za udhibiti, leseni na usajili kwa watoa huduma za usafiri majini.
Kupitia mfumo huu, watoa huduma wataweza kuomba leseni na vyeti vya usajili, kuwasilisha nyaraka zinazohitajika, kufuatilia hatua za maombi yao na kupata taarifa mbalimbali kwa njia ya mtandao. Hatua hii itapunguza matumizi ya nyaraka za karatasi pamoja na muda unaotumika katika kufuatilia huduma kwa njia ya kawaida.
Mfumo wa MTRS ni hatua muhimu katika kuboresha na kuimarisha huduma za udhibiti wa sekta ya usafiri majini nchini Tanzania.
Mafunzo hayo yanatarajiwa kufika kuhitimishwa tarehe 28 Agosti, 2026.