Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

TASAC YAENDELEA KUTOA ELIMU KATIKA MAONESHO YA WIKI YA MADINI GEITA

Imewekwa: 27 September, 2026
TASAC YAENDELEA KUTOA ELIMU KATIKA MAONESHO YA WIKI YA MADINI GEITA

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) linaendelea kushiriki katika Maonesho ya Wiki ya Madini yanayofanyika kuanzia tarehe 23 Septemba hadi 03 Oktoba 2026 katika Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Bombambili, Mkoani Geita.

Kupitia ushiriki wake katika maonesho hayo, TASAC inapata fursa ya kuwafikia wananchi na wadau mbalimbali na kutoa elimu kuhusu majukumu, huduma na shughuli zinazotekelezwa na Shirika katika sekta ya usafiri wa majini nchini.

Aidha, TASAC inatumia maonesho hayo kutoa tahadhari kwa wananchi na wadau kuhusu matarajio ya mvua za Vuli zinazotarajiwa kuanza wiki ya nne ya mwezi Septemba hadi Desemba 2026, ambazo zinatarajiwa kuathiriwa kwa kiwango kikubwa na El Niño. Tahadhari hiyo inalenga kuwakumbusha wadau kuhusu umuhimu wa kuzingatia usalama wakati wa shughuli za usafiri wa majini, pamoja na kufuata sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia sekta hiyo.

TASAC linawakaribisha wananchi na wadau wa Mkoa wa Geita na maeneo ya jirani kutembelea banda la Shirika katika eneo la maonesho ili kupata taarifa zaidi kuhusu majukumu, huduma na shughuli mbalimbali za TASAC, pamoja na namna linavyoshirikiana na wadau katika kuendeleza sekta ya usafiri wa majini nchini.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo