TASAC NA LiMA WASAINI HATI YA MAKUBALIANO YA KUSHIRIKIANA KATIKA MASUALA YA USAFIRI MAJINI
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Majini ya nchini Liberia (LiMA) wamesaini hati ya makubaliano ya kushirikiana katika masuala ya usafiri majini, leo tarehe 13 Februari, 2026 katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jiiini Dar Es salaam.
Makubaliano hayo yamesainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Bw.Mohamed Salum na Mheshimiwa Robert Wilmort, Balozi mwakilishi wa Kudumu wa Liberia katika Shirika la Bahari Duniani (IMO).
Mkubaliano haya yatasaaidia TASAC na LiMA kujifunza kwa kubalishana uzoefu wakusimamia usalama na ulinzi wa meli zinazosafiri katika maji ya Kimataifa,
Kubadilishana utaalam wa usajiri wa meli katika jukumu la kutekelwza mikataba ya Kimataifa inayosimamiwa na Shirika la Bahari Duniani, na
Aidha, mabaharia wa Tanzania watapata fursa ya mafunzo ya vitendo kwenye meli zilizosajiriwa nchini Liberia.