Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

NAIBU BALOZI WA KENYA NCHINI TANZANIA ATEMBELEA BANDA LA TASAC SABASABA

Imewekwa: 11 July, 2026
NAIBU BALOZI WA KENYA NCHINI TANZANIA ATEMBELEA BANDA LA TASAC SABASABA

Naibu Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Bw. Mohamed Hussein, tarehe 9 Julai 2026 alitembelea Banda la Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA), ambapo alipokelewa na Meneja wa Rasilimali Watu wa TASAC, Bi. Pili Mazowea.

Katika ziara hiyo, Mhe. Hussein alipata fursa ya kujionea shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na TASAC pamoja na elimu inayotolewa kwa wananchi kuhusu sekta ya usafiri wa majini.

Kupitia maonesho hayo, maafisa wa TASAC walimueleza majukumu ya Shirika, ikiwemo kudhibiti usafiri na usafirishaji wa majini, kusimamia usalama, ulinzi na utunzaji wa mazingira katika sekta ya usafiri wa majini, kusajili na kutoa vyeti kwa mabaharia,  kusimamia biashara za meli, pamoja na kuhamasisha uzingatiaji wa sheria na kanuni zinazoratibu sekta hiyo.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo